Friday, June 15, 2012

KUTANA NA DOUGLAS PIUS(DP). MTANGAZAJI ANAYEPIGANIA KUKUBALIKA KWA HIPOP GOSPEL TANZANIA.




Douglas Pius(DP) ni mtangazaji wa kituo cha radio cha praise power kilichopo Mikocheni B Dar-es-salaam Tanzania.Harakati zake za utangazaji zilianzia mkoani Mbeya ambapo alianza kutangaza kupitia kituo cha radio kijulikanacho kama BOMBA FM.Na baada ya muda alihamia katika kituo cha radio ya kidini ijulikanayo kama BARAKA FM ipatikananyo jijini Mbeya na kuzidi kufanya vizuri zaidi mpaka ikapelekea kuchukuliwa na radio ya PRAISE POWER kinachomilikiwa na kanisa la Mikocheni B Assemblise of God.
    Kabla hajaokoka DP alikuwa anafanya muziki wa Rap hivyo alivyookoka aliendelea kulinyanyua jina la Yesu kwa njia ya HIPOP GOSPEL.

     Kwasasa amefanikiwa kuanzisha kipindi cha HIPOP GOSPEL kupitia kituo cha PRAISE POWER na kipindi icho  kinalushwa kila siku ya jumamosi kuanzia saa 10 za jioni mpaka saa 1 za usiku.

2 comments:

  1. namkubal sana jembe langu

    ReplyDelete
  2. Safi sana DP, we need to make every effort to make sure Jesus is exalted, all Music is for God. For his glory.

    ReplyDelete